Mama, Hivi Ndivyo Mwili Wako Unavyopona Baada ya Kujifungua

Imekaguliwa kitabibu na Midwife Rhoda James Kallabaka, 2026-09-16.

Umefika nyumbani na mtoto, na kila mtu anauliza habari zake. Sisi tunaanza na wewe.

Kwa mama aliyejifungua kawaida

Lochia: Ni kawaida kutokwa damu kwa wiki kadhaa. Huanzia nyekundu, kisha hupungua na kubadilika kuwa pinki/kahawia hadi njano-nyeupe.

Mshono au mchaniko: Weka eneo safi na kavu, badilisha pedi mara kwa mara na epuka kusugua eneo la mshono.

Choo cha kwanza: Kunywa maji, kula vyakula vyenye fibre na usisukume kwa nguvu. Choo kikiwa kigumu kwa siku kadhaa, wasiliana na kliniki.

Kwa mama aliyejifungua kwa upasuaji (C-section)

Lochia: Utatokwa damu pia, hata kama hukujifungua kupitia uke. Damu inapaswa kupungua taratibu kadri siku zinavyokwenda.

Kidonda: Kiweke safi na kikavu kulingana na maelekezo ya hospitali. Wekundu unaoongezeka, usaha, harufu mbaya, homa au maumivu yanayozidi yanahitaji kuangaliwa.

Movement: Anza kutembea taratibu kadri unavyoweza, lakini epuka kujilazimisha au kubeba vitu vizito wakati mwili bado unapona.

Kwa mama wote

Maumivu ya tumbo kama ya hedhi yanaweza kutokea wakati kizazi kinarudi kwenye ukubwa wake wa kawaida. Jasho la usiku na baby blues pia vinaweza kutokea wiki za mwanzo.

Dalili za tahadhari

Nenda hospitali haraka ukiona:

Kumbuka: Recovery ni process. Wewe pia unahitaji kutunzwa.