Mama, Zijue Haki Zako Wakati wa Kujifungua
Imekaguliwa kitabibu na Midwife Rhoda James Kallabaka, 2026-09-16.
Haki Zako Wakati wa Kujifungua
Kila mama anastahili huduma salama, yenye heshima na inayomshirikisha katika maamuzi. Kujua haki zako si ugomvi; ni sehemu ya usalama wako.
Haki ya Kuelezwa na Kukubali
Una haki ya kuambiwa nini kinafanyika na kwa nini—iwe dawa, kipimo, kuchochewa uchungu, episiotomy au upasuaji. Kuuliza “Hii ni ya nini?” ni haki yako.
Kwenye dharura: Ikiwa wewe au mtoto mko kwenye hatari ya haraka, timu ya afya inaweza kuhitaji kufanya maamuzi na kutoa huduma kwa haraka. Inapowezekana, utaelezwa kinachoendelea na sababu yake.
Haki ya Heshima na Faragha
Una haki ya kutendewa kwa heshima, utu na faragha, bila kudhalilishwa kwa sababu ya kulia, kupiga kelele au jinsi unavyopitia uchungu.
Msindikizaji
Inapendekezwa mama awe na msindikizaji anayemchagua wakati wa labour na kujifungua. Taratibu zinaweza kutofautiana kwa kila hospitali, hivyo uliza mapema.
Ukihisi Huduma Si Sawa
Uliza mhudumu anayekuhudumia. Usipoelewa au kuridhika, omba kuzungumza na msimamizi wa zamu na tumia utaratibu wa malalamiko wa kituo inapohitajika.
Kumbuka
Fika na taarifa zako za kliniki, toa historia yako kwa ukweli na uliza chochote usichoelewa.
Fanya leo: Chagua msindikizaji wako mapema na mjadili support unayotaka wakati wa labour na kujifungua.