Labor & Delivery: Nini Hutokea Hatua kwa Hatua?
Imekaguliwa kitabibu na Midwife Rhoda James Kallabaka, 2026-09-16.
Hofu kubwa ya kujifungua mara nyingi huongezwa na kutojua nini kinakuja baada ya nini. Hii ni ramani rahisi ya hatua za uchungu hadi mtoto kuzaliwa.
Hatua ya kwanza: uchungu unaanza na kujijenga
Mwanzoni mikazo inaweza kuwa midogo na isiyo na mpangilio, kama maumivu ya hedhi yanayokuja na kuondoka. Hatua hii inaweza kuchukua masaa mengi, hasa kwa mama anayejifungua kwa mara ya kwanza.
Kama umeambiwa ujauzito wako hauna tatizo na hospitali haijakupa maelekezo tofauti, unaweza kutumia muda huu kupumzika, kula na kunywa, kuoga na kutembea taratibu.
Mlango wa kizazi (cervix) hufunguka polepole hadi kufikia sentimita 10. Kasi si sawa kwa kila mama—kusikia “bado 4 cm” haimaanishi mwili wako umeshindwa.
Tumia Kipima Mikazo kufuatilia mikazo yako. Kanuni ya 5-1-1—mikazo karibu kila dakika 5, kila mmoja ukidumu takribani dakika 1, kwa karibu saa 1—inaweza kuwa mwongozo wa kuwasiliana au kuelekea hospitali, lakini fuata pia maelekezo uliyopewa na kituo chako.
Uchungu unapokuwa mkali zaidi
Kadri mlango unavyokaribia kufunguka kabisa, contractions kuwa kali**, kudumu mda mrefu na kuwa karibu karibu zaidi.** Unaweza kuhisi umechoka sana, kutetemeka, kuwa na pressure kubwa au kusema “siwezi tena.”
Hapa support ni muhimu. Pumua kati ya mikazo, badilisha position kadri unavyoweza, na msindikizaji au mkunga akusaidie kukaa focused.
Kusukuma: mtoto anakaribia
Mlango wa kizazi ukifunguka kabisa (10 cm), unaweza kuhisi pressure kubwa chini, wakati mwingine kama unataka kwenda chooni.
Mkunga atakuongoza kulingana na hali yako na ya mtoto. Muda wa kusukuma hutofautiana—kwa baadhi ni mfupi, kwa wengine unaweza kuchukua muda zaidi, hasa kwa mtoto wa kwanza.
Kuhusu episiotomy (kupanua njia kwa kukata sehemu ndogo ya msamba), haipaswi kufanywa routinely kwa kila mama; hufanyika pale inapohitajika kitabibu.
Baada ya mtoto: placenta inatoka
Mtoto akishazaliwa bado kuna hatua moja—placenta (kondo la nyuma) kutoka. Mikazo midogo huendelea kusaidia placenta kutoka na kizazi kukaza.
Kwa kawaida dawa ya kusaidia kizazi kukaza, mara nyingi oxytocin, hutolewa ili kupunguza hatari ya kutokwa damu nyingi baada ya kujifungua.
Kama hali ya mama na mtoto inaruhusu, huu pia ni muda wa skin-to-skin, kumweka mtoto kifuani na kuanza kunyonyesha mapema.
Usisubiri contractions pekee
Nenda au wasiliana na hospitali haraka ukivuja maji, una damu nyingi, mtoto anacheza kidogo kuliko kawaida, una maumivu makali yasiyopungua kati ya mikazo, au umepewa maelekezo maalum kutokana na hali ya ujauzito wako.
Fanya leo: Kamilisha begi lako na mpango wako, kisha soma kuhusu kupunguza maumivu.