Miguu kuvimba wakati wa Ujauzito
Imekaguliwa kitabibu na Midwife Rhoda James Kallabaka, 2026-09-16.
Uvimbe wa Miguu Kwenye Ujauzito: Normal au Warning Sign?
Uvimbe wa miguu ni common wakati wa ujauzito, hasa miezi ya mwisho. Lakini wakati mwingine unaweza kuwa warning sign ya pre-eclampsia.
Uvimbe wa Kawaida
Miguu na ankles (vifundo) vikivimba taratibu, hasa jioni, baada ya kusimama muda mrefu au wakati wa joto, mara nyingi ni kawaida.
Ili kupunguza uvimbe:
Inua miguu unapopumzika
Epuka kusimama muda mrefu
Vaa viatu comfortable
Kunywa maji ya kutosha
Fanya movement nyepesi kama kutembea
Pre-eclampsia
Pre-eclampsia ni hali ambapo pressure (BP) hupanda wakati wa ujauzito, mara nyingi baada ya wiki 20, na inaweza kuleta complications kwa mama na mtoto.
Warning signs:
Uvimbe wa ghafla, hasa usoni na mikononi
Kichwa kikali kisichoisha
Kuona ukungu au vimulimuli
Maumivu makali juu ya tumbo/chini ya mbavu
Kutapika ghafla au kujisikia vibaya sana
Ukiona dalili hizi, tafuta huduma ya afya haraka.
Kwa Nini BP na Mkojo Hupimwa Clinic?
Pre-eclampsia inaweza kuanza bila dalili. Ndiyo maana BP na mkojo huangaliwa kwenye antenatal clinic. Usikose clinic visits hata kama unajisikia vizuri.
Nani Yuko Kwenye Risk Zaidi?
Risk inaweza kuwa juu zaidi kwa pregnancy ya kwanza, mapacha, aliyewahi kupata pre-eclampsia, au mwenye high BP, diabetes au kidney disease.
Kwa baadhi ya walio high risk, healthcare provider anaweza ku-prescribe low-dose aspirin. Usianze mwenyewe bila maelekezo.
Inatibiwaje?
Management inaweza kujumuisha kufuatilia BP na mtoto, dawa inapohitajika, na kupanga muda salama wa kujifungua.
Kumbuka: Uvimbe sio kila mara pre-eclampsia. Lakini uvimbe wa ghafla pamoja na headache kali, vision changes au maumivu chini ya mbavu usipuuzwe.