Ovulation Calculator

Imekaguliwa kitabibu na Midwife Rhoda James Kallabaka, 2026-08-05.

Ovulation: Siku Zako za Kushika Mimba

Ovulation ni wakati yai linapotoka kwenye ovary na kuwa tayari kurutubishwa. Hiki ndicho kipindi ambacho nafasi ya kupata mimba huwa juu zaidi.

Ovulation Inahesabiwaje?

Kwa cycle ya siku 28, ovulation mara nyingi hutokea karibu siku ya 14, ukihesabu kuanzia siku ya kwanza ya hedhi.

Lakini si kila mwanamke ana cycle ya siku 28. Njia rahisi ya kukadiria ni:

Chukua tarehe unayotarajia period inayofuata, kisha hesabu nyuma takribani siku 14.

Mfano: Kama period yako inayofuata inatarajiwa tarehe 28, ovulation inaweza kuwa karibu tarehe 14.

Fertile Window ni Nini?

Fertile window ni takribani siku 6: siku 5 kabla ya ovulation pamoja na siku ya ovulation.

Chance ya kupata mimba huwa kubwa zaidi unapofanya tendo karibu na siku za ovulation.

Signs za Ovulation

Unaweza kuona:

Unawezaje Kujua Kwa Usahihi Zaidi?

Calendar ni makadirio, hasa kama cycle zako haziko regular. Unaweza pia kutumia ovulation predictor kit (OPK) au kufuatilia cervical mucus na basal body temperature.

Kumbuka: Haya ni makadirio tu, si tarehe ya uhakika ya ovulation. Cycle inaweza kubadilika mwezi hadi mwezi, hasa kama periods zako si regular.