Ultrasound: nini kinaangaliwa
Imekaguliwa kitabibu na Midwife Rhoda James Kallabaka, 2026-09-16.
Ultrasound Wakati wa Ujauzito
Kwa wengi, ultrasound ndiyo mara ya kwanza ya “kumwona” mtoto kabla hajazaliwa. Lakini pia huja na maswali mengi: Ni salama? Nifanye lini? Inaangalia nini?
Ni salama, na si mionzi
Ultrasound hutumia mawimbi ya sauti, si X-ray wala radiation. Inapotumika kitabibu na kufanywa na mtaalamu, inachukuliwa kuwa salama wakati wa ujauzito.
Nifanye lini?
Mapema kwenye pregnancy: inaweza kusaidia kujua umri wa mimba, due date, idadi ya watoto na kuthibitisha pregnancy ilipo.
Wiki 18–22: hapa ndipo mara nyingi hufanyika anatomy scan kuangalia ukuaji na maumbile ya mtoto kama moyo, ubongo, uti wa mgongo na viungo vingine.
Trimester ya tatu: inaweza kufanyika ikihitajika kufuatilia ukuaji, maji au position ya mtoto.
Na jinsia? 👀
Inaweza kuonekana, lakini si guarantee. Inategemea wiki za pregnancy na position ya mtoto. Akikaa position inayoficha sehemu zake, unaweza kutoka bila jibu. 😅
Kumbuka, kazi kubwa ya ultrasound si kujua jinsia tu, bali kufuatilia maendeleo ya mtoto.
3D/4D ni lazima?
Hapana. Inaweza kukupa picha nzuri zaidi ya mtoto, lakini si lazima kwa kila pregnancy. Medical ultrasound inayoshauriwa na mtoa huduma wako ndiyo muhimu zaidi.
Kumbuka Mama ❤️
Ultrasound ni zaidi ya picha ya mtoto. Inasaidia healthcare team kufuatilia pregnancy na maendeleo ya mtoto wako.
Kama hujui ultrasound yako inayofuata ni lini, uliza kwenye clinic visit yako inayofuata.