Kila Mtoto Ana Kasi Yake:Lakini Hizi Dalili Usizipuuze

Imekaguliwa kitabibu na Midwife Rhoda James Kallabaka.

Usiharakishe kumlinganisha mtoto wako na wengine. Watoto hawafikii kila hatua siku moja, lakini kuna hatua muhimu tunazotarajia kadri wanavyokua.

Baadhi ya hatua muhimu

Karibu miezi 2, mtoto huanza kutabasamu unapoongea au kumtabasamia. Kufikia miezi 9, watoto wengi wanaweza kukaa bila kusaidiwa. Kufikia miezi 18, wengi hutembea bila kushikilia na hujaribu kusema maneno kadhaa zaidi ya “mama” au “dada.”

Mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati anaweza kufuatiliwa kwa umri uliorekebishwa (corrected age) badala ya umri wa kuzaliwa pekee.

Lini uongee na mtaalamu?

Ongea na mtaalamu ikiwa mtoto hafikii hatua zinazotarajiwa kwa umri wake, una wasiwasi kuhusu jinsi anavyocheza, kuongea, kusikia au kutembea, au amepoteza uwezo aliokuwa nao tayari. Usisubiri kuona kama “atajifunza mwenyewe”—kuangaliwa mapema kunaweza kusaidia kujua kama anahitaji msaada zaidi.

Msaidie kila siku

Ongea naye, mwimbie, msomee na cheza naye. Haya ni mambo rahisi yanayosaidia mtoto kujifunza na kujenga uhusiano na watu wanaomzunguka.

Kumbuka: Usimlinganishe na mtoto mwingine; fuatilia hatua zake kulingana na umri wake na uliza kliniki unapokuwa na wasiwasi.