Kuanza Chakula kwa Mtoto wa Miezi 6
Imekaguliwa kitabibu na Midwife Rhoda James Kallabaka.
Mpaka miezi sita, maziwa ya mama pekee yanatosha kwa mtoto anayenyonya hata maji hahitaji. Miezi sita ikifika, mtoto anahitaji virutubisho zaidi kutoka kwenye chakula, huku kunyonyesha kukiendelea hadi miaka miwili au zaidi.
Chakula gani cha kuanzia?
Anza na kiasi kidogo cha chakula kilichopondwa na kisicho chepesi kama maji. Uji unaweza kuwa mwanzo, lakini usiwe chakula pekee.
Mpe vyakula tofauti kama maharage, dagaa au samaki wasio na mifupa, nyama, yai lililoiva vizuri, viazi vitamu, ndizi, parachichi, papai na mboga. Kadri anavyozoea, ongeza aina na texture ya chakula.
Usijali sana kuhusu “chakula cha kwanza perfect.” Muhimu ni mtoto kupata vyakula vya aina tofauti, hasa vyenye iron kama nyama, samaki, yai na maharage. Unaweza pia kuchanganya chakula: kwa mfano viazi vitamu na maharage yaliyopondwa, au uji mzito pamoja na chakula kingine chenye virutubisho.
Nianze na kiasi gani?
Siku za mwanzo mtoto bado anajifunza kula, kwa hiyo anaweza kula vijiko vichache tu. Hilo ni kawaida. Anza kidogo na ongeza taratibu kulingana na hamu yake.
Usipime mafanikio kwa bakuli kuisha. Mtoto akifunga mdomo, kugeuza kichwa au kupoteza interest, anaweza kuwa ameshiba. Mhimize, lakini usimlazimishe kumaliza chakula.
Kunyonyesha kunaendelea kama kawaida. Kuanzisha chakula hakumaanishi maziwa ya mama yanasimamishwa ghafla.
Kadri anavyokua
Miezi 6–8: anza na kiasi kidogo cha chakula laini mara 2–3 kwa siku.
Miezi 9–11: ongeza texture—chakula kinaweza kupondwa au kukatwakatwa laini. Mpe milo 3–4 kwa siku, na snack inapohitajika.
Mwaka 1+: anaweza kuanza kula chakula cha familia kilichoandaliwa kwa namna salama kwake, pamoja na snacks zenye lishe. Kunyonyesha kunaendelea.
Usikae muda mrefu sana na chakula kilichosagwa laini kabisa. Kadri mtoto anavyoweza kula vizuri, ongeza texture taratibu ili ajifunze kutafuna na kushughulikia vyakula tofauti.
Vipi kuhusu yai, karanga na vyakula vya allergy?
Vyakula vinavyoweza kusababisha allergy kama yai lililoiva vizuri na karanga katika hali salama kama peanut butter laini iliyochanganywa kwenye chakula vinaweza kuanzishwa baada ya mtoto kuanza complementary foods; si lazima kusubiri mpaka mwaka mmoja.
Anza kiasi kidogo na uwe makini na reaction. Mtoto akipata uvimbe wa uso au midomo, shida ya kupumua, au reaction kali baada ya chakula, tafuta huduma ya afya haraka.
Kama mtoto ana eczema kali au allergy inayojulikana, zungumza na mtaalamu kuhusu kuanzisha vyakula hivi.
Makosa ya kuepuka
Uji mwepesi sana: mtoto anahitaji chakula chenye lishe na consistency nzuri, si maji mengi.
Asali kabla ya mwaka 1: usimpe kabisa; inaweza kusababisha ugonjwa hatari unaoitwa infant botulism.
Kulazimisha kula: mpe muda na jaribu chakula tena siku nyingine. Mhimize kula, lakini usimlazimishe.
Soda, pipi na vyakula vyenye sukari nyingi: havihitajiki kwa mtoto. Pia usiongeze sukari au chumvi kwenye chakula chake.(chumvi ya kuongezaa badaa ya kupakua chakula)
Vyakula vinavyoweza kumkwamisha: karanga nzima, zabibu nzima na vipande vigumu vya chakula vinaweza kusababisha choking. Chakula kiandaliwe kulingana na uwezo wa mtoto kula.
Gagging na choking si kitu kimoja
Mtoto anapojifunza kula anaweza kukohoa, kutoa sauti au kusukuma chakula nje ya mdomo—hii inaweza kuwa gagging na ni sehemu ya kujifunza kula.
Lakini choking ni tofauti: mtoto anaweza kushindwa kupumua, kukohoa au kutoa sauti. Hii ni emergency. Ndiyo maana mtoto anapaswa kula akiwa amekaa wima na chini ya uangalizi wa mtu mzima kila wakati. Usimlishe akiwa amelala, anatembea au anacheza.
Maji na usafi
Kuanzia miezi 6, mtoto anaweza kupewa maji safi kwenye kikombe. Osha mikono, tumia vyombo safi na andaa chakula kwa usafi ili kupunguza hatari ya kuhara.
Usihifadhi chakula kilichobaki kwenye bakuli ambalo mtoto tayari amekula bila kuzingatia usalama wa chakula—mate yanaweza kuingiza vijidudu kwenye chakula.
Kumbuka: Miezi sita haimaanishi kuacha maziwa ya mama. Chakula kinaongezeka taratibu huku kunyonyesha kukiendelea. Mwanzo si kuhusu mtoto kula sahani nzima; ni kuhusu kujifunza kula, kuonja vyakula tofauti na kujenga lishe nzuri hatua kwa hatua.