Kupata Mtoto: Si Kila Unachosikia Ni Kweli

Imekaguliwa kitabibu na Midwife Rhoda James Kallabaka, 2026-09-16.

Kipindi cha kutafuta ujauzito kina ushauri mwingi lakini si kila unachosikia ni kweli.

1. “Uzazi wa mpango unasababisha ugumba”

Ukweli: Njia nyingi za uzazi wa mpango hazisababishi ugumba wa kudumu. Uwezo wa kupata ujauzito hurudi baada ya kuacha, ingawa kwa sindano unaweza kuchelewa kwa muda.

2. “Lazima ulale chali baada ya tendo”

Ukweli: Hakuna ushahidi kwamba kulala chali baada ya tendo kunaongeza nafasi ya kupata ujauzito. Mbegu huanza kusafiri kuelekea kwenye kizazi haraka baada ya tendo.

3. “Tatizo la kushika ujauzito ni la mwanamke”

Ukweli: Sababu zinaweza kutoka kwa mwanamke, mwanaume, wote wawili, na wakati mwingine sababu haipatikani. Ndiyo maana uchunguzi unaweza kuwahusisha partners wote wawili.

4. “Ili ushike, lazima mfanye tendo kila siku”

Ukweli: Si lazima. Kufanya tendo kila siku moja au mbili katika siku zenye nafasi kubwa ya kupata ujauzito kunatosha.

5. “Dawa za kusafisha kizazi zinasaidia kupata ujauzito”

Ukweli: Hakuna ushahidi kwamba dawa za “kusafisha kizazi” zinaongeza nafasi ya kupata ujauzito. Baadhi zinaweza hata kuwa na madhara.

6. “Usiposhika mwezi wa kwanza, kuna tatizo”

Ukweli: Kupata ujauzito kunaweza kuchukua muda hata kama hakuna tatizo la uzazi. Kutopata ujauzito mwezi wa kwanza hakumaanishi kuna tatizo.

Kumbuka: Unaposikia ushauri kuhusu fertility, hakikisha unatoka kwenye chanzo cha afya kinachoaminika.