Wakati Sahihi wa Kupima Mimba na Kutafuta Msaada
Imekaguliwa kitabibu na Midwife Rhoda James Kallabaka, 2026-09-16.
Maswali mawili makubwa kwa wanaojaribu kupata ujauzito: nipime lini, na nitafute msaada lini?
Lini kupima mimba
Pima kuanzia siku ya kwanza hedhi inapochelewa. Ukipima mapema sana unaweza kupata negative hata kama una mimba. Ikiwa ni negative lakini hedhi haiji, rudia baada ya siku chache.
Msaada baada ya muda gani?
Kwa partners wanaojaribu kupata ujauzito bila mafanikio, muda wa kufanya uchunguzi wa uzazi hutegemea umri wa female partner:
Chini ya miaka 35: baada ya miezi 12.
Miaka 35–40: baada ya miezi 6.
Zaidi ya miaka 40: ni vyema kuanza uchunguzi wa uzazi mapema zaidi.
Usisubiri kama...
Hedhi haiji au haiko regular, una maumivu makali ya hedhi, una historia ya matatizo yanayoweza kuathiri uzazi (kama PID), au mmoja wa partners ana tatizo la uzazi linalojulikana. Katika hali hizi, uchunguzi unaweza kuanza mapema bila kusubiri miezi 6 au 12.
Vipimo vinaanzaje?
Uchunguzi unawahusu partners wote wawili inapohusika. Unaweza kujumuisha historia ya afya, semen analysis, uchunguzi wa ovulation, ultrasound na vipimo vingine kulingana na hali.
TTC (Trying to Conceive) ni kipindi cha kujaribu kupata ujauzito. Kama mmefikia muda huu, zungumzeni na mtaalamu wa afya ili kuanza uchunguzi wa uzazi pamoja