Mambo 7 ya Kufanya Kabla ya Kupata Ujauzito
Imekaguliwa kitabibu na Midwife Rhoda James Kallabaka, 2026-09-16.
Safari ya mtoto huanza kabla ya ile mistari miwili. Maandalizi kabla ya ujauzito yanaweza kuboresha afya yako na kusaidia kumpa mtoto mwanzo wenye afya.
1. Anza folic acid mapema
Tumia folic acid 400 mcg kila siku, kuanzia angalau mwezi mmoja kabla ya ujauzito. Husaidia kuzuia baadhi ya kasoro kubwa za ubongo na uti wa mgongo, ambazo huanza kutokea wiki za mwanzo kabisa za ujauzito.
2. Pima sickle cell
Ni vizuri wewe na partner wako kupima sickle cell kabla ya kupata ujauzito. Kipimo hiki husaidia kujua kama mmoja au wote wawili mnabeba vinasaba vya sickle cell. Kama wote wawili ni AS, kila ujauzito una nafasi ya 25% ya mtoto kuwa na sickle cell (SS). Kujua mapema kunawasaidia kupata ushauri sahihi.
3. Dhibiti hali zako za kiafya
Una BP ya juu, kisukari, pumu au unatumia dawa kila siku? Ongea na mtaalamu kabla ya ujauzito. Baadhi ya dawa au matibabu yanaweza kuhitaji kurekebishwa.
4. Jilinde dhidi ya malaria
Anza kutumia chandarua chenye dawa kila usiku. Kujikinga na malaria ni muhimu kabla na wakati wa ujauzito.
5. Acha pombe na sigara
Kwa anayeweza kupata ujauzito, ni salama zaidi kuacha pombe unapojaribu kupata ujauzito. Sigara pia huathiri afya na inaweza kupunguza fertility. Partner naye anapaswa kuzingatia afya yake.
6. Jenga lifestyle yenye afya
Lenga chakula balanced, movement ya mara kwa mara na uzito wenye afya. Uzito wa chini sana au mkubwa unaweza kuathiri fertility na afya ya ujauzito.
7. Jiandaeni kama timu
Afya ya partner pia ni muhimu fertility haihusu mwanamke pekee. Ongeleeni afya, lifestyle na maandalizi ya kupata mtoto pamoja.
Fanya leo: Anza folic acid na panga preconception check-up ili kujua maandalizi yanayokufaa wewe na partner wako.