Afya ya Uzazi wa Mwanaume: Upande Tunaousahau

Imekaguliwa kitabibu na Midwife Rhoda James Kallabaka, 2026-09-16.

Kwenye safari ya kutafuta mtoto, mwanaume mara nyingi husahaulika. Lakini afya yake ya uzazi ni sehemu muhimu ya kupata ujauzito. Male factor inaweza kuchangia peke yake au pamoja na sababu nyingine.

Mbegu zinahitaji muda

Kutengenezwa kwa mbegu ni mchakato unaochukua takriban miezi 2–3. Ndiyo maana kujenga lifestyle yenye afya mapema ni muhimu.

Linda afya yako

Acha sigara, punguza pombe, kula vizuri, fanya mazoezi na pata usingizi wa kutosha. Pia epuka joto kali la muda mrefu kwenye korodani.

Hakuna supplement au “dawa ya kuongeza mbegu” inayofaa kwa kila mwanaume—tatizo likiwepo, ni bora kujua chanzo chake kwanza.

Lini mwanaume apime?

Kama ujauzito haujapatikana baada ya miezi 12 ya kujaribu, au miezi 6 ikiwa female partner ana miaka 35 au zaidi, partners wote wanapaswa kufanyiwa uchunguzi. Kwa mwanaume, semen analysis ni sehemu muhimu ya uchunguzi wa mwanzo.

Safari ni ya wawili

Kutafuta mtoto si jukumu la mwanamke pekee. Kujali afya yako, kushiriki maamuzi na kwenda kwenye uchunguzi pamoja ni sehemu ya safari pia.

Fanya leo: Kama unavuta sigara au una lifestyle unayotaka kubadilisha, anza sasa—afya yako ya uzazi nayo inastahili care.