je mama akijifungua kwa c, section anaweza kuanza kufunga tumbo baada ya mda gani?

Majibu (2)

Jibu la @rhoda8092 (mtaalamu aliyethibitishwa)

Mama aliyejifungua kwa upasuaji (C-section) anashauriwa kuanza kufunga tumbo kati ya siku ya 7 hadi ya 10 baada ya upasuaji

, kipindi ambacho kidonda kwa kawaida huwa kimepona kwa nje. Kabla ya kuanza, ni muhimu kuhakikisha kidonda kimefunga vizuri na ni kikavu. Endapo kidonda bado hakijapona, kiko wazi, au kinatoa majimaji au usaha, tumbo lisifungwe. Mama arudi hospitali aonwe kwanza. Kila mama hupona kwa kasi yake, hivyo ushauri wa daktari aliyemhudumia ndio wa kufuata. Daktari akitoa maelekezo tofauti na haya, maelekezo yake yazingatiwe.

Jibu la @mama3823

asanteeee

Jiunge na Malkia Circle ujibu au uulize swali lako