Jibu la @rhoda8092 (mtaalamu aliyethibitishwa)
Baada ya kujifungua, mama anapaswa kupata huduma zifuatazo: - Kupimwa shinikizo la damu na kuangaliwa kiasi cha damu inayotoka ukeni.
- Kukaguliwa vidonda na kuhakikisha mfuko wa uzazi unasinyaa vizuri. - Kupata msaada na maelekezo kuhusu unyonyeshaji. - Kupata ushauri kuhusu lishe, usafi na mapumziko. - Kupata huduma za afya ya akili na ushauri wa uzazi wa mpango. Mama anashauriwa kupata uchunguzi ndani ya saa 24, siku ya 2–3, siku ya 7–14 na wiki ya sita baada ya kujifungua. Endapo atapata homa, damu nyingi ukeni, maumivu makali ya kichwa au tumbo, uchafu wenye harufu mbaya au shida ya kupumua, anapaswa kuwahi hospitalini. Rhoda James Kalabaka Registered Midwife