Nawezaje kuongeza uzalishaji wa maziwa??

Weeks mbili sasa kiwango cha maziwa ni kidogo na mtoto hashibi akinyonya. Nimejaribu kila njia yaongezeke

Majibu (1)

Jibu la @rhoda8092 (mtaalamu aliyethibitishwa)

Pole Faith. Njia inayofanya kazi kuliko zote ni kunyonyesha mara nyingi zaidi: angalau mara 10 kwa saa 24, usiku pia

, matiti yote mawili kila mara. Usimwongezee maji, uji wala maziwa ya kopo, kwa sababu yanapunguza maziwa yako. Kwa kuwa umejaribu njia nyingi na bado hashibi, mpeleke kliniki wiki hii apimwe uzito na waangalie anavyoshika titi. Mara nyingi tatizo ni jinsi anavyonyonya, si kiasi cha maziwa.

Jiunge na Malkia Circle ujibu au uulize swali lako