Jibu la @rhoda8092 (mtaalamu aliyethibitishwa)
Wewe: milo mitatu na vitafunwa viwili kwa siku, kila mlo uwe na protini (maharage, mayai, samaki au dagaa) na mboga za majani.
Endelea na dawa zako za kliniki. Mtoto wa miezi 18: chakula cha familia mara tatu kwa siku, vitafunwa viwili, na maziwa. Kama bado ananyonya unaweza kuendelea, ila mwambie mkunga wako kliniki. Punguza kumbeba, na pumzika kila anapolala.