Ni dalili zipi zinazoashiria kuwa mama mjamzito anatakiwa kwenda hospitali haraka?

Majibu (1)

Jibu la @rhoda8092 (mtaalamu aliyethibitishwa)

Mama mjamzito anapaswa kwenda hospitalini haraka endapo atapata mojawapo ya dalili zifuatazo: - Kutokwa na damu ukeni.

- Maumivu makali ya tumbo. - Maumivu makali ya kichwa au kuona ukungu. - Kuvimba ghafla kwa uso na mikono. - Mtoto kupunguza au kuacha kucheza tumboni. - Kutokwa na maji ya uzazi. - Homa kali au kutetemeka. - Kupata degedege au kupoteza fahamu. - Kupumua kwa shida au maumivu ya kifua. - Kupata uchungu kabla ya kutimiza wiki 37 za ujauzito. Dalili hizi zinaweza kuashiria hatari kwa afya ya mama au mtoto. Ni muhimu kuwahi hospitalini bila kusubiri miadi inayofuata ya kliniki. Rhoda James Kalabaka Registered Midwife

Jiunge na Malkia Circle ujibu au uulize swali lako