Jibu la @rhoda8092 (mtaalamu aliyethibitishwa)
Ndiyo mama! ❤️ Kutembea wakati wa ujauzito kunaweza kusaidia mwili kujiandaa kwa ajili ya kujifungua kawaida (vaginal delivery).
Faida zake ni: Huimarisha misuli na stamina ya mwili. Husaidia kuboresha mzunguko wa damu. Movement inaweza kusaidia mtoto kujiposition vizuri kwenye nyonga. Husaidia kupunguza stress na kuboresha usingizi. Ushauri wa mkunga: Tembea dakika 20–30 kwa siku kama ujauzito wako hauna changamoto za kiafya. Kumbuka mama, kutembea hakuhakikishi kujifungua kawaida, lakini kunaweza kusaidia mwili wako kujiandaa.